Exodus 22:21-24

21“Usimtendee mgeni vibaya au kumwonea, kwa kuwa nanyi mlikuwa wageni huko Misri.

22 a“Usimdhulumu mjane wala yatima. 23 bKama ukifanya hivyo nao wakinililia, hakika nitasikia kilio chao. 24 cHasira yangu itawaka, nami nitawaua kwa upanga, wake zenu watakuwa wajane na watoto wenu watakuwa yatima.

Copyright information for SwhKC